Tuesday, August 27, 2013

Udereva.

Tags

Udereva.

Sifa za Mwombaji:-

 • Awe Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 • Awe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 25.
 •  Awe amemaliza kidato cha nne au cha sita na kufaulu.
 •  Awe amemaliza kidato cha nne na kuendelea katika kipindi cha mwaka 2010, 2011 au 2012.
 •  Awe na cheti cha ufundi magari(Automobile engineering au Transport Management and logistics) yaani NTA level 2 au 3 au 4
 •  Awe na leseni ya udereva daraja “D”, “E” au “C”.
 •  Awe na cheti halisi cha kuzaliwa, kuhitimu elimu ya sekondari, na cheti cha taaluma.
 •  Awe na tabia njema na asiwe na kumbukumbu za uhalifu.
 •  Awe na afya njema itakayothibitishwa na daktari wa Serikali.
 •  Awe hajaoa, hajaolewa au kuwa na mtoto.
 •  Asiwe na alama za kuchora mwilini(Tatuu).
 •  Awe na urefu usiopungua sentimita 155.
 •  Awe hajawahi kutumia madawa ya kulevya.
 •  Awe amefaulu usaili.
 •  Awe tayari kufanyakazi mahali popote Tanzania.


Jeshi la Polisi Tanzania katika mwaka wa fedha 2013/2014 litaajiri wahitimu wa vyuo vya Ufundi Stadi nchini na Vyuo vya Mafunzo ya Amali Zanzibar.
Wahitimu wa fani hizo wawasilishe maombi yakiambatanishwa na vivuli vya vyeti kwa Inspekta Jenerali wa Polisi, Makao Makuu ya Polisi, S. L. P. 9141, Dar es Salaam kwa kujaza fomu ya maombi iliyowekwa kwenye tovuti ya Jeshi la Polisi www.policeforce.go.tz Fomu za maombi baada ya kupokelewa, zitachambuliwa wenye sifa wataitwa kwenye usaili kwa tarehe zitakazotangazwa kwenye vyombo vya habari. Baada ya usaili majina ya waliofaulu yatatangazwa na watatakiwa kuhudhuria mafunzo ya awali katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi. 

Muhimu: Mwisho wa kupokelewa kwa fomu za maombi ni tarehe 15.09.2013.
Hairuhusiwi kuwasilisha fomu ya maombi kwa mkono. Tuma kwa 
posta kupitia anuani tajwa.