-->

Friday

Fisheries Assistant II – Nafasi 18


Published by Jobstanzania on 12:46:00 am

Mvuvi Msaidizi Daraja La II (Fisheries Assistant II) – Nafasi 18

Majukumu Ya Kazi

 • · Kutengeneza, Kushona, Kutunza na Kukarabati zana za uvuvi.
 • · Kutunza na kuangalia mabwawa ya samaki.
 • · Kutega mitego Ziwani au Baharini.
 • · Kutengeneza nyavu ndogo ndogo.
 • · Kuwapa chakula samaki katika mabwawa.
 • · Kuvua samaki katika mabwawa.
 • · Kutoa ushauri kwa wavuvi kuhusu mbinu mbalimbali za uvuvi.
 • · Kukusanya takwimu za uvuvi kutoka kwenye vituo vya kupokelea samaki.
 • · Kutoa ushauri juu ya uhifadhi wa samaki na mbinu za usambazaji na uuzaji wa
 • mazao yatokanayo na samaki.
 • · Kuwaelimisha wananchi juu ya ufugaji wa samaki na mambo muhimu ya
 • kuzingatia.

Sifa Za Mwombaji
 • · Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au cha sita wenye stashahada (Diploma) ya Uvuvi au Uhifadhi wa Samaki na Masoko (Fish Processing & Marketing) kutoka vyuo vya uvuvi vya Mbegani, Kunduchi au vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
Mshahara
· Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS C kwa mweziMashariti ya Jumla Kwa Kazi Zote
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania.
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za
kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe katika kichwa cha habari cha barua na juu
ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye
anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika.
vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya
kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya
kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho
hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka kupotea.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vii. “Transcripts”, “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”,
hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS
SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
viii. Waombaji wawe na umri usiozidi miaka 45.
ix. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba
isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
x. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko
katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo
yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za
kisheria.
xiii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 12 Desemba, 2013
xiv. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira
HAURUHUSIWI.
xv. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe
kupitia posta kwa anuani ifuatayo.

Katibu, ,
Sekretariati ya Ajira katika 
Utumishi wa Umma, 
S.L.P 63100, 
Dar es Salaam. 


Share/Bookmark

 


Web Analytics