-->

Tuesday

Afisa utumishi II (TGS D) - Nafasi 80


Published by Jobstanzania on 11:02:00 am

Tume ya Utumishi wa Mahakama ni chombo kilicho undwa kwa mujibu wa aya ya 112 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1997. Aidha kwa mujibu wa sheria ya uendeshaji wa mahakama Na. 4/2011, Tume ya Utumishi wa mahakama mbali na kuwa na majukumu mengine, inalo jukumu la kuajiri watumishi wa kada mbalimbali wa Mahakama.

Hivyo tume ya utumishi wa mahakama inawatangazia watanzania wenye sifa zilizo ainishwa hapo chini kwa kila nafasi ya kazi na ambao wapo tayari kufanya kazi katika Ofisi za Mahakama ya Tanzania ambazo zipo katika mikoa na wilaya mbalimbali kuleta maombi yao ya kazi.

Afisa utumishi II (TGS D) - Nafasi 80

Sifa:
Shahada ya kwanza ya sayansi ya jamii au sanaa kutoka katika Vyuo Vikuu vinavyo tambulika na serikali ambao wamejiimarisha (major) katika mojawapo ya fani zifuatazo:-

- Menejimenti ya rasilimali watu (Human resource management)
- Elimu ya jamii (Sociology)                                                         
- Utawala na Uongozi (Public Administration)                           
- Mipango ya watumishi (Manpower planning)                         
- Wawe na ujuzi wa kutumia kompyuta.         
                           
Waombajin watapangiwa kazi Mahakama za wilaya isipokuwa za mkoa wa Dar es salaam. Waombaji wa nafasi hii waonyeshe wilaya tatu (3) zilizopo katika mojawapo ya mikoa ifuatayo: Pwani, Morogoro, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Njombe, Iringa, Mbeya, Rukwa, Katavi, Kigoma, Tabora, Simiyu, Mara, Mwanza, Geita, Kagera, Singida, Dodoma, Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga na Shinyanga ambazo wangependa kupangiwa ingawa pendekezo lao linaweza lisizingatiwe. Aidha, baadaye watabadilishwa kazi kuwa watendaji wa Mahakama.

Kazi za Afisa utumishi Daraja la II

(i) Kutunza kumbukumbu sahihi za watumishi wote.
(ii) Kutafsiri na kushughulikia miundo ya utumishi.
(iii) Kutafiti, kuchanganua, kupanga, na kukadiria idadi ya watumishi wanao hitaji mafunzo.
(iv) Kukusanya, kuchambua, na kupanga takwimu na kumbukumbu zote zinazohusu mipango ya watumishi.
(v) Kushughulikia masuala mbalimbali ya kila siku ya watumishi.
(vi) Kusimamia OPRAS

Mwisho wa kupokea barua za maombi ni Tarehe 16/02/2015 saa 9:30 Alasiri.

Barua za maombi ziandikwe kwa mkono wa mwombaji na kuambatanisha:-
- Vivuli vya vyeti vyote vya elimu na mafunzo.
- Ufupisho wa taarifa za mwombaji (CV)
- Kivuli cha cheti cha kuzaliwa.
- Picha mbili (Passport size) zilizopigwa hivi karibuni.

Waombaji walio katika utumishi wa Umma wanapaswa kupitisha maombi yao kwa waajiri wao na walio wahi kuacha kazi katika utumishi wa Umma waeleze bayana kuwa waliacha kazi katika utumishi wa Umma.

Maombi yote yatumwe kwa njia ya Posta kwa Katibu, Tume ya Utumishi wa Mahakama ya Tanzania,

Katibu,
Tume ya Utumishi wa Mahakama,
S.L.P 8391,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA.


Share/Bookmark

 


Web Analytics