-->

Monday

Nafasi 15 za Kazi Halmashuri ya Wilaya ya Kilolo


Published by Jobstanzania on 2:23:00 pm

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo amepokea kibali cha ajira chenye kumb Na. FA/71/363/01/38 cha tarehe 31/07/2017 pamoja na kibali Kumb Na. FA/170/363/01/48 cha tarehe 22/09/2017 aidha kufuatia vibali hivyo mkurugenzi Mtendaji anawatangazia wananchi wote wenye sifa za kujaza nafasi za kazi zifuatazo

1. MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA II – NAFASI 1

SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu elimu ya kidato cha Sita/Nne na Mafunzo ya Astashahada/Diploma katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Dodoma, au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

KAZI ZA KUFANYA

 • Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji.
 • Kusimamia ulinzi na Usalama wa raia na mali zao.
 • Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Kijiji.
 • Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji.
 • Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu.
 • Kuandaa Taarifa za Utekelezaji wa kazi katika eneo lake na Kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali.
 • Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na Nyaraka za Kijiji.


MSHAHARA
TGS C1 – Tshs 525, 000/= hadi Tshs 668,000/=2. MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III – NAFASI 9

Awe amehitimu elimu ya kidato cha Sita/Nne na Mafunzo ya Astashahada/Cheti katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Dodoma, au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

KAZI ZA KUFANYA

 • Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji.
 • Kusimamia ulinzi na Usalama wa raia na mali zao.
 • Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Kijiji.
 • Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji.
 • Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu.
 • Kuandaa Taarifa za Utekelezaji wa kazi katika eneo lake na Kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali.
 • Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na Nyaraka za Kijiji.


MSHAHARA
TGS B1 – Tshs 390, 000/= hadi Tshs 489,000/=


3. DEREVA DARAJA LA II - NAFASI 5


SIFA ZA MWOMBAJI

 • Mwenye cheti cha Mtihani wa kidat cha IV, 
 • Wenye Lseni daraja la “C” uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa mda usiopungua miaka mitatu bila kusababisha ajali, 
 • wenye cheti cha majaribio ya Ufundi Daraja la II Watafikiriwa kwanza


KAZI NA MAJUKUMU
1. Kuendesha magari ya abiria na malor
2. Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote, na kufanya uchunguzi wa gari kabla na baada ya safari ili kugundua ubovu unaohitajika matengenezo
3. Kufanya matengenezo madogo madogo katika gari
4. Kutunza na kuandika daftari la safari “Log book” kwa safari zote

MSHAHARA
TGS B1 – Tshs 390, 000/= hadi Tshs 489,000/=MAMBO YA KUZINGATIA

 • mwombaji awe raia wa Tanzania
 • awe na umri kati ya miaka 18 hadi 45
 • barua zote ziandikwe kwa mkono na ziambatanishwe na nyaraka zifuatazo
 • maelezo binafsi
 • nakala za vyeti vya kidato cha 4 au 6 cheti cha kuzaliwa na vyeti vya elimu ya taluma
 • picha ndogo 2 passport size za hivi karibuni
 • transcript, testimonial results havitakubaliwa
 • mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 09/03/2018
 • maombi yatakayoletwa baada ya muda ulowekwa katika tangazo hayatopokelewa
 • tangazo hili linapatikana kwenye tovuti ya Halmashauri www.kilolodc.go.tz

Barua zitumwe kwa

MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA YA KILOLO,
S.L.P 2324,
KILOLO.


Share/Bookmark

 


Web Analytics