Wednesday, July 17, 2019

MKUSANYA MAPATO (Nafasi 20) - DART

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka, anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi wazi ishirini na nne (24) kama zilivyobainishwa katika tangazo hili.


MKUSANYA MAPATO (Nafasi 20) 

SIFA ZA MUOMBAJI.
Awe na elimu ya Kidato cha nne na amehitimu elimu ngazi ya cheti katika fani zifuatazo (Uhasibu, Biashara, Manunuzi, Takwimu, Hisabati) kutoka chuo vinachotambuliwa na Serikali.


MAJUKUMU YA KAZI.
i. Kukusanya fedha zote katika maegesho ya magari pamoja na sehemu za huduma ya choo,
ii. Kukusanya takwimu za magari yanayoegeshwa kwa siku pamoja na takwimu za watumiaji wa choo kwa siku,
iii. Kuandaa hesabu za makusanyo ya kila siku kwa kutumia fomu za RCCB,
iv. Kutunza fedha zote za makusanyo ya siku na kuhakikisha Usalama wa fedha hizo kabla hazijafika ofisini,
v. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na Elimu, uzoefu na ujuzi wake.MASHARTI YA JUMLA

i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania,
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa,
iii. Waombaji wote wawe na umri kuanzia miaka 18 hadi 45,
iv. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)watatu wa kuaminika.
v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya kidato cha nne, taaluma, kwa wale waliohitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika waambatanishe vyeti vya mafunzo husika.
vi. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA
vii. Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni.
viii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na Baraza la Mitihani Tanzania – (NECTA).
ix. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Maombi yote yatumwe kwa: -
MTENDAJI MKUU,
WAKALA WA MABASI YAENDAYO HARAKA,
S.L.P 724,
DAR ES SALAAM.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 24 Julai, 2019.

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAKUBALIWA.